KURA 2017: SERIKALI YA TAIFA YA RWANDA INAYOTUMIKIA UHAMISHONI INATULIZA WANANCHI WA RWANDA

KURA 2017: SERIKALI YA TAIFA YA RWANDA INAYOTUMIKIA UHAMISHONI INATULIZA WANANCHI WA RWANDA

Kwa muda usiopita miezi sita, Serikali ya taifa ya Rwanda iliyo uhamishoni itakuwa imepiga marufuku « Miungu » inayokaliya kiti kwa nguvu nchini Rwanda.

Baada ya kutazama kwa makini namna nchi yetu ya Rwanda inaongozwa tukota tarehe ya 1/10/1990 kufika saa hii; na kugundua kuwa watu wanazingatiwa na misiba mbalimbali, hali ya wasiwasi kwa kila mwananchi kwa sababu ya serikali mbaya inayoongozwa na Paul Kagame ambaye anaendelea kujitambua kama « Katili asiye na huruma, Jambazi na Muuaji wa wengi aliyehifadhiwa na kinga ya urais, Mwendawazimu anayetaka kuombwa kama Miungu ya zamani »,

I. Hebu tukakumbuke kwanza hatua tulizochukua hadi leo :

1.Tarehe 28/1/13 , Abataripfana ( jina la kikundi chetu linayomaanisha wasioogopa kusema ukweli)  walikutania Paris nchini Ufaransa na kuanza Chama cha kisiasa chenye jina la ISHEMA RY’U RWANDA . Chama hicho kilikuwa na mradi wa kujivunia kuwa wanyarwanda na kukataa kuwa watumwa nchini mwao;

2.Punde si punde Vyama vingine vya vijana (New Generation parties) viliunga mkono Chama cha Ishema kwa mradi wa kurudi Rwanda na kujiunga na wananchi wenzetu kwa kujenga nchi kimawazo na kimaendeleo;

3. Tulichukua mda usiwo mfupi wa kuongea, kufikiria, kufanya mijadala na wataalamu tofauti , kufanya ziara kwa nchi za kigeni na kuongea na wakimbizi kwenye nchi waliko mahali pengi duniani.

4. Tulitembelea nchi za kirafiki na kuzieleza mradi wetu waliofurahia na kukubali kutuunga mkono wakati tutakapofika Rwanda.

5. Timu yetu ya kwanza ilijitayarisha kutoka uhamishoni na kwenda Rwanda. Ilikuwa inaongozwa na Padri Thomas Nahimana aliyekua amechaguliwa kama mugombea wa kiti cha urais wa Chama cha Ishema , mwezi wa Ogusti 2017.

6. Tulisikitika sana kuona mradi wetu mzuri wenye amani na fanaka haukutendeka kwa saabu ya Katili Kagame aliyechukua hatua ya kusimamisha mgombea wa urais Thomas Nahimana na wanachama waliokuwa na yeye. Hiki kitendo haramu kilifanyika mara mbili : Kwa kiwanja cha ndege cha Nairobi tarehe 21/11/2016 na 31/1/2017 Ubeligiji.

7. Isikike vizuri kuwa KAGAME hakukuwa na nia nyingine isiyo « kuogopa » kuwa  wananchi wa Rwanda wako tayari kumchaguwa rais mpya  na kukataa « mfalme Kagame » wakati wa kura tarehe ya 3-4/8/2017;

II.Kwa kuwa ubaya wa Paul Kagame umevuka mpaka, leo tunataka kutangazia wenzetu wanyarwanda na Ulimwengu  maoni yetu yafuatayo :

1. Serikali ya taifa ya Rwanda iliyo uhamishoni inayoshirikiana inakataa kabisa matokeo ya upigaji kura uliotendeka tarehe ya 3-4/8/2017, kwa sababu wagombea kiti cha urais wengine walikatazwa kupigiwa kura bila sababu yeyote. Kwa mfano : Diane Rwigara na Mwenedata Gilbert;

2. Hata hivyo, tunajulisha watu wote kuwa Kagame Paul si rais wa nchi ya Rwanda kwa sababu wakati wa mamlaka wake uliisha tarehe ya 3/8/2017. Saa hii hana uwezo wowote kisheria.

3.Tunahakikisha kuwa serikali mpya anayejitayalisha kuunda  haina tofauti na  « Kundi la Majambazi yenye bunduki »  na nia yake ni kutesa wananchi na kuwaongoza kama vipofu.

4.Paul Kagame tulimuomba mara kadhaa kuachia huru wafungwa wa kisiasa kama : Ingabire Victoire, Deogratias Mushayidi, Padri Edwaridi Nturiye , Padri Amatus Mategeko…akajifanya kiziwi. Hakuna kusisitiza kwingine tena.

5.Serikali ya taifa ya Rwanda iliyo uhamishoni inasikitishwa na mateso ya wananchi wote, na ina matumaini kwamba itafanya viwezekanavyo ili wakati wa miezi sita kutoka sasa ikuwe imepata mbinu za kupiga marufuku « Kundi la Majambazi yenye bunduki  » yaliyotufanya watumwa nchini mwetu.

6.Tunaomba wananchi wote kwa ujumla na watu kibinafsi kutuunga mkono ili mradi wetu wa kujitoa kwa mikono ya « Kundi la majambazi » tuufikie kwa urahisi.

7.Tunashukuru viongozi vya nchi za kirafiki waliotuonyesha kuwa wanasikitishwa na uwizi na ukatili wa Paul Kagame. Tunawashukuru pia kwa kutuhakikisha kwamba wao ni tayari kutuunga mkono ili mwananchi wa Rwanda wapate uhuru na amani.

8.Tunaomba Shirika ya kimataifa kutusikia na kutusaidia kwa hatua hii isiyo rahisi ya kutupilia mbali « Serikali ya Kundi la Majambazi » na kuyichukulia vikwazo kali  vya kisheria, kiuchumi, kisiasa na kijeshi ili Majambazi waondoke wananchi wajichaguliwe rais wanaomtaka.

Mungu ayibaliki Rwanda na Wanyarwanda !

Paris, Agosti, 2017
Padri Thomasi Nahimana
Rais

 

 

 

One thought on “KURA 2017: SERIKALI YA TAIFA YA RWANDA INAYOTUMIKIA UHAMISHONI INATULIZA WANANCHI WA RWANDA

  1. Ishyaka rishya ryavuutse ishakwe ;RNC new , Inkubiri

Comments are closed.

Comments are closed.